1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi amuokoa kocha mpya wa Barcelona

20 Januari 2020

Barcelona walicheza mechi yao ya kwanza baada ya kumuachisha kazi kocha wao Ernesto Valverde na walikuwa na mkufunzi mpya Quique Setien na shukran kwa Lionel Messi waliweza kupata ushindi wa moja bila dhidi ya Granada.

Champions League 2019 | FC Barcelona vs. Borussia Dortmund | Lionel Messi & Antoine Griezmann
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Monfort

Ushindi huo unawaweka kileleni mwa La Liga wakiwa na alama arubaini na tatu sawa sawa na mahasimu wao Real Madrid ila Madrid wameshindwa na tofauti ya mabao. Atletico Madrid wanaishikilia nafasi ya tatu na Sevilla ni wa nne wote wakiwa na pointi thelathini na tano.

Baada ya kuulizwa anachostahili kurekebisha katika kikosi chake, kocha mpya wa Barca Quique Setien alikuwa na haya ya kusema.

"Timu imecheza vyema, nikitulia na kuitazama tena mechi nina uhakika nitaona vitu tunavyostahili kuvirekebisha lakini kwa ujumla ninafurahishwa na mambo mengi tuliyoyaona leo, labda tunaweza kucheza kwa kusambaza mpira zaidi unapokuwa uwanjani lakini nitalitazama hilo kwa undani zaidi," alisema Setien.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW