Messi apiga hatrick Kombe la Dunia
17 Juni 2026
Matangazo
Mechi za Kombe la Dunia 2026 zinaendelea kutimua vumbi katika mataifa ya Marekani,Mexico na Canada. Katika mchezo uliomalizika asubuhi hii mabingwa watetezi wa michuano hii Argentina wameichaaza Algeria 3-0. Magoli yote yakitiwa kimiani na Lionel Messi ambaye sasa ameifikia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo Miroslav Klose ya mabao 16.
Katika mechi za awali, mabingwa wa dunia 2018 Ufaransa walitembeza kichapo kwa Senegal kwa magoli 3-1. Nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappe akitia wavuni mabao mawili na kuweka rekodi mpya ya kufikisha magoli 14 katika michuano hiyo.
Norway nayo wameicharaza Iraq magoli 4-1 huku Erling Halland akitupia kambani magoli mawili.