Messi asaini mkataba mpya na Inter Miami
18 Septemba 2025
Kwa mujibu wa chanzo kilichokaribu na klabu ya Inter Miami, Mkataba huo mpya unahakikisha kuwa Messi, mwenye umri wa miaka 38, ataendelea kushiriki mashindano ya kiwango cha juu hadi na baada ya Kombe la Dunia litakalofanyika Marekani, Kanada na Mexico. Mashindano hayo yataanza Juni 11 na fainali kufanyika Julai 19 katika Uwanja wa MetLife.
Mkataba wa awali wa Messi ulikuwa unamalizika mwishoni mwa mwaka huu baada ya kukamilika kwa msimu wa ligi ya MLS wa 2025. Tangazo rasmi linatarajiwa ndani ya wiki mbili zijazo, na huenda likamaanisha Messi atastaafu soka akiwa Inter Miami.
Huku haya yakiarifiwa, Benfica wamethibitisha leo Alhamisi kuwa wako katika mazungumzo ya kumwajiri Jose Mourinho kama kocha wao mpya.
Hii na ya Benfica kumfuta kazi kocha Bruno Lage baada ya kushindwa nyumbani kwa mabao 3-2 dhidi ya Qarabag ya Azerbaijan katika mechi ya Ligi ya Mabingwa.