1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi kubaki Barca au kutimkia kwingine?

Admin.WagnerD17 Mei 2021

Wakati msimu wa Barcelona umemakimilika bila kubeba ubingwa wa La Liga, Lionel Messi ana uamuzi muhimu wa kufanya. Je, amalize taaluma yake ya kandanda katika klabu hiyo iliyomsaidia kuwa mchezaji bora ulimwenguni?

Fußball Lionel Messi FC Barcelona
Picha: Christophe Ena/AP/picture alliance

Wakati msimu wa Barcelona umemakimilika bila kubeba ubingwa wa La Liga, Lionel Messi ana uamuzi muhimu wa kufanya. Je, amalize taaluma yake ya kandanda katika klabu hiyo iliyomsaidia kuwa mchezaji bora ulimwenguni? Au kutokana na kuyumba kwa timu hiyo kumemshahiwishi kutafuta mafanikio Paris au Manchester? Barcelona waliondolewa katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa Uhispania baada ya kupigwa 2 – 1 na Celta Vigo.

Atletico Madrid iliipiga Osasuna 2 – 1 na sasa wanaweza tu kukamatwa na Real Madrid katika duru ya mwisho wa msimu wikiendi ijayo. Real iliifunga Athletic Bilbao 1 – 0. Ubingwa wa Laliga utaamuliwa wikiendi ijayo kati ya watani wa mjini Atletico na Real.

Ubingwa wa Ligue 1 kuamuliwa siku ya mwisho

Kama tu ilivyo nchini Uhispania, ubingwa wa ligi kuu Ufaransa Ligue 1 utaamuliwa wikiendi ijayo kati ya Lille na Paris Saint German. PSG ilipata ushindi wa 4 – 0 dhidi ya Reims, wakati Lille ikilazimishwa sare tasa na Saint-Etienne na kupunguza hadi pointi moja mwanya kati yao na nambari mbili PSG. Timu zite mbili zitacheza ugenini wikiendi ijayo ambapo PSG wataangushana na Brest na Lille wakabiliane na Angers.

Tuchel bado ana imani na wachezaji wake

Nchini England, Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amesema hajapoteza Imani kwa wachezaji wake kufuatia kichapo cha Jumamosi cha 1 – 0 katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Leicester City. Amesema watajipanga upya na kupambana kujikatia tiketi ya kumaliza katika nne bora kwenye Premier League na kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chelsea ipo katika nafasi ya nne na pointi 64, pointi mbili nyuma ya Leicester City na moja tu juu ya Liverpool huku ikiwa imebaki mechi mbili msimu kumalizika. Kesho jumanne, vijana hao wa Tuchel watacheza dhidi ya Leicester na lengo la kulipiza kisasi.

AFP/Reuters/DPA/AP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW