MEXICO CITY: Vimbunga vinavuma Mexico na Marekani
1 Septemba 2006Matangazo
Kimbunga “John” kilichovuma nje ya pwani ya Mexico upande wa bahari ya Pacifik,kimesababisha mvua kubwa,kikielekea Baja California.Kwa sababu ya kimbunga hicho chenye mwendo wa kilomita 205 kwa saa,wakazi na watalii wa Kimarekani wamehamishwa kutoka eneo hilo la pwani.Wakati huo huo kwenye pwani ya mashariki ya Marekani, kimbunga “Ernesto” kinazidi kuwa na nguvu baada ya kuvuka eneo la kusini la Florida.Jumapili iliyopita “Ernesto” kilikuwa kimbunga cha kwanza kuvuma katika eneo la Atlantik.
