1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO CITY:Benki ya dunia kuendelea bila ya Venezuela

17 Juni 2007

Anaetarajiwa kuwa rais wa benki ya dunia bwana Robert Zoelllick amesema kuwa benki hiyo haitapoteza uzito wake ikiwa Venezuela itajitoa kwenye benki hiyo.

Akizungumza na waandishi habari mjini Mexico City bwana Zoellick ameahidi kurejesha heshima ya shirika hilo baada ya kujiuzulu rais wa hapo awali bwana Wolfowitz kutokana na kashfa.

Bodi ya wakurugenzi 24 ya benki hiyo inatarajiwa kumchagua bwana Zoellick baadae mwezi huu kuchukua nafasi ya bwana Wolfowitz.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW