1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMexico

Mexico: Mafuriko makubwa na maporomoko yasababisha vifo

12 Oktoba 2025

Mamlaka nchini Mexico imesema watu wapatao 41 wamekufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi kwenye eneo la kusini mashariki la nchi hiyo.

Mexiko Poza Rica 2025 | Mafuriko nchini Mexico kutokana na mvua kubwa
Athari ya Mafuriko nchini Mexico iliyosababishwa na mvua kubwaPicha: Rolando Ramos/REUTERS

Juhudi za kuwasaidia waliokumbwa na maafa zinaendelea huku serikali ikiwa imewapeleka wanajeshi elfu 10 kwenye eneo lililoathirika. 

Kwa mujibu wa taarifa watu wengine 27 bado hawajulikani walipo. Mafuriko na maporomoko ya adhri makubwa yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la kusini mashariki mwa Mexico.

Mamlaka ya Mexico imesema mpaka sasa ni vigumu kuwafikishia maalfu ya watu misaada kwa sababu ni shida kuvifikia vijiji vingi vilivyoathirika na maafa hayo. Wataalamu wa hali ya anga wameonya kuwa mvua zaidi zinatarajiwa kunyesha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW