1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMexico

Mexico yamchagua Sheinbaum kuwa rais wa kwanza mwanamke

3 Juni 2024

Mgombea wa chama tawala cha Morena nchini Mexico Claudia Sheinbaum amechaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke katika ushindi wa kishindo jana Jumapili.

Rais Mteule wa Mexico Claudia Sheinbaum
Rais Mteule wa Mexico Claudia SheinbaumPicha: Eduardo Verdugo/AP Photo/picture alliance

Sheinbaum baada ya matokeo hayo aliwashukuru wafuasi wake waliomchagua na kuwaahidi kutowaangusha.

Mwanamama huyo ambaye ni mwanasayansi mwenye umri wa miaka 61 alitabiriwa kushinda kwa kati ya asilimia 58 hadi 60 ya kura, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Uchaguzi. Ushindi huo ni asilimia 30 dhidi ya mpinzani wake Xochilt Galvez, ambaye pia ni mwanamke, na karibu asilimia 50 mbele ya Jorge Alvarez Maynez, mwanaume pekee aliyegombea urais.

Inakadiriwa asilimia 60 ya watu walijitokeza kupiga kura nchini Mexico kati ya watu milioni 100 waliojiandikisha.