1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mexico yasitisha uhusiano na balozi za Marekani na Canada

28 Agosti 2024

Mexico imesimamisha uhusiano na mabalozi wa Marekani na Canada, lakini siyo na nchi hizo. Mexico imechukua hatua hiyo baada ya mabalozi wa Marekani na Canada kuelezea wasiwasi juu ya mabadiliko ya Mexico.

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez ObradorPicha: Mexican Presidency/Handout/AFP

Mexico imesimamisha uhusiano na mabalozi wa Marekani na Canada, lakini siyo na nchi hizo. Mexico imechukua hatua hiyo baada ya mabalozi wa Marekani na Canada kuelezea wasiwasi juu ya mabadiliko makubwa ambayo Mexico inakusudia kuyafanya katika mfumo wake wa sheria. Mexico imevunja uhusiano wa kidiplomasia na Ecuador baada ya maafisa kuuvamia ubalozi wake

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador, ameeleza kwamba hatua iliyochukuliwa na nchi yake inawahusu mabalozi wa nchi hizo mbili na siyo nchi zao. Wiki iliyopita balozi wa Marekani nchini Mexico Ken Salazar, alisema mabadiliko katika mfumo wa sheria  ambayo Mexico inakusudua kuyafanya yatahatarisha demokarsia na mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hiyo na Marekani. Rais wa Mexico amesema, kwa kauli hiyo balozi wa Marekani amejiingiza katika mambo ya ndani ya Mexico.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW