Meya wa New York akana mashitaka ya ufisadi
28 Septemba 2024Matangazo
Adams mwenye umri wa miaka 64, amekuwa meya wa kwanza wa mji huo mkubwa wa Marekani kushtakiwa akiwa mamlakani.
Baadaye Jaji Katharine Parker aliamuru kuachiliwa kwa afisa huyo huku akimkataza kuwasiliana na mashahidi waliotajwa kwenye hati ya mashtaka.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Jumatano wiki ijayo, na wakili wa Eric Adams, Alex Spiro , ameahidi kuwa atawasilisha ombi la kuyafuta mashtaka hayo.