Najma Juma ni mwigizaji anayechipuka kwa kasi katika tasnia ya filamu. Kwa kipaji cha kipekee na juhudi zisizo na kikomo, amekuwa akivutia macho ya watazamaji na wataalamu wa filamu. Ingawa ni mpya kwenye tasnia, licha ya juhudi zake amekuwa akikumbana na changamoto kubwa ya kukatishwa tamaa katika mitandao ya kijamii lakini kwake anaitumia kama chachu ya kufikia malengo yake.
Kipindi hiki kinakupa fursa ya kusikia ujasiri wa msichana na mchango mkubwa anaoufanya katika jamii. Msichana Jasiri ni muwazi, ana upendo na yuko tayari kujitoa kuwahudumia wengine. Ni shujaa!