Mfalme Abdullah akataa pendekezo la kuwahamisha Wapalaestina
12 Februari 2025
Matangazo
Hii ni baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, aliyetoa wito wa wakazi hao karibu milioni 2 kuondolewa kwenye eneo hilo lililoharibiwa na vita.
Kwenye mkutano na Trump, Abdullah alijitolea kuwachukua hadi watoto 2,000 kutoka Gaza wenye maradhi ya saratani ama wanaohitaji huduma za dharura za matibabu.
Lakini baada ya mkutano huo, kupitia mtandao wa X aliandika ujumbe akisisitiza msimamo mkali wa Jordan dhidi ya hatua ya kuwahamisha Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi. Akaongeza kuwa huo ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya kiarabu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit pia amelipinga wazo hilo akiliita lisilokubalika kwenye ukanda huo, huku China ikisema Gaza ni ya Wapalestina.