1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Uingereza na Ufaransa zaombwa kuimarisha mahusiano yao

21 Septemba 2023

Mfalme Charles III wa Uingereza aliye ziarani nchini Ufaransa ametoa rai kwa mataifa hayo mawili washirika kuyapiga jeki zaidi mahusiano yao ili kukabiliana na changamoto za karne ya 21

Mfalme Charles  III akiwa ziarani mjini Paris
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mfalme Charles III wa Uingereza Picha: Christian Hartmann/REUTERS

Akizungumza wakati ya hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na mwenyeji wake rais Emmanuel Macron, Mfalme Charles amesema mahusiano ya Ufaransa na Uingereza yameshuhudia kipindi cha msukusuko lakini ni wajibu wa nchi hizo mbili kuyaimarisha tena . 

Ingawa Mfalme Charles hakulitaja moja kwa moja suala la Brexit ambalo limekuwa chanzo cha mgawanyiko kati ya Uingereza na mataifa washirika wa Ulaya, alisema lakini Uingereza na Ufaransa zimekuwa na historia ndefu iliyojaa vizingiti. 

Kwa upande wake rais Macron amemhakikishia mFalme Charles kuwa licha ya Uingereza kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya bado itaendelea kuwa sehemu ya kanda hiyo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za pamoja.

Ziara ya Mfalme Charles nchini Ufaransa ilianza hapo jana mchana na itamalizika kesho Ijumaa.