1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUingereza

Mfalme Charles III wa Uingereza agunduliwa na saratani

6 Februari 2024

Utawala wa Kifalme nchini Uingereza umetangaza kuwa Mfalme Charles III amegunduliwa kuwa na saratani ambayo hata hivyo haikuelezwa wazi ni aina gani.

Uingereza- Mfalme Charles III akiwa na mkewe Malkia Camilla
Mfalme Charles III (kushoto) akiwa na mkewe Malkia Camilla katika Kasri la Kifalme la Buckingham jijini London: 06.05.2023Picha: LEON NEAL/AFP

Mamlaka ya Kasri la Buckingham imeeleza kuwa saratani hiyo iligundulika wakati wa matibabu ya kawaida ya tezi dume na kwamba kwa sasa Mfalme huyo ameanza kupatiwa matibabu na atahitaji kupumzika.

Viongozi mbalimbali duniani wakiwemo rais wa Marekani Joe Biden, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na wengine kadhaa, wametuma  salamu za kumtakia ahueni Mfalme huyo aliyechukua madaraka baada ya kifo cha mama yake Malkia Elisabeth mnamo Septemba 8 mwaka 2022, aliyeiaga dunia akiwa na umri wa miaka 96.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW