1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles wa Uingereza azomewa Australia

21 Oktoba 2024

Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza amezomewa na mbunge wa jamii ya wenyeji wa Autralia katika ziara yake nchini humo. Mfalme huyo wa Uingereza na mkewe, Malkia Camilla, wameutembelea mji mkuu wa Australia, Canberra.

Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza na mkewe Camilla
Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza na mkewe CamillaPicha: Mark Baker/AP Photo/picture alliance

Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza amezomewa na mbunge wa jamii ya  wenyeji wa Autralia katika ziara yake nchini humo.

Mbunge huyo, Lidia Thorpe, alimwambia Mfalme Charles kwamba Australia siyo nchi yake. Aliishutumu Uingereza kwa mauaji ya halaiki yaliyofanywa na wakololoni nchini Australia. Mbunge anayejulikana kwa kupinga ukoloni wa Australia alipaza sauti na kusema turudishie ardhi yetu Charles, alipomaliza kulihutubia Bunge.

Soma: Mfalme Charles III azungumzia maandamano ya vurugu Uingereza

Mfalme Charles yuko katika ziara yake rasmi ya 16 nchini Australia na safari yake ya kwanza kuu ya nje tangu kugundulika kuwa na saratani.

Mfalme huyo wa Uingereza na mkewe, Malkia Camilla, wameutembelea mji mkuu wa Australia, Canberra, leo. Ziara hiyo ya siku sita, ambayo ilianza Ijumaa, ni ya kwanza kwa mfalme huyo tangu awe mkuu wa nchi hiyo ya Jumuiya ya Madola mnamo mwezi Septemba 2022.