1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme wa Moroko tayari kuutatuwa mkwamo wa Sahara Magharibi

12 Oktoba 2024

Mfalme Mohammed IV wa Moroko amethibitisha kwamba kuutatuwa mzozo wa muda mrefu wa mamlaka ya Sahara Magharibi kunaendelea kuwa suala muhimu kwenye siasa za nje za ufalme huo wa kaskazini mwa Afrika.

Moroko | Mfalme Mohammed IV
Mfalme Mohammed IV wa MorokoPicha: Alexander Shcherbak/TASS/dpa/picture alliance

Akitoa hotuba yake ya kila mwake bungeni hapo jana, Mfalme huyo alisema uamuzi wa Marekani, Uhispania na Ufaransa kutambuwa mamlaka ya Moroko kwa Sahara Magharibi umechangia kuonesha uwezekano wa kupatikana kwa suluhu mapema zaidi.

Moroko inaichukulia Sahara Magharibi kuwa jimbo lake la kusini, lakini kwa muda wote wakaazi wa eneo hilo wanajitambuwa kuwa taifa tafauti wanaloliita Sahrawi, likiongozwa na chama cha ukombozi cha Polisario.

Soma zaidi: Maelfu waandamana Moroco kushinikiza kusitishwa mahusiano na Israel

Uamuzi wa mataifa ya Magharibi kuitambua Moroko kuwa na mamlaka ya eneo hilo, unahusishwa na kukubali kwa Mfalme Mohammed wa Nne kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Israel mnamo mwaka 2020.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW