1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme wa Ubelgiji ajutia maovu ya ukoloni kwa Wakongomani

Jean Noël Ba-Mweze, DW, Kinshasa. 9 Juni 2022

Mfalme Filipo wa Ubelgiji amejutia maovu Wabelgiji waliwatendea Wakongomani enzi za ukoloni. Amesema hayo akiwahutubia wabunge na maseneta wa Kongo huko Kinshasa katika ziara yake ya wiki moja.

King Philippe - Filip of Belgium stands still at a wreath laying at the Memorial aux anciens combattants , in Kinshasa,
Picha: Benoit Doppagne/BELGA/IMAGO

Mfalme Filipo amekiri kuwa wakoloni walitenda mabaya mengi. Halafu amejutia kuhusu mambo hayo ila hakuomba msamaha. 

"Utawala wa kikoloni ulijikita katika unyonyaji uliofikilia kutozwa ada na fedheha. Mbele ya  wakongomani na wale ambao bado wanateseka hadi leo, ninathibitisha tena majuto yangu makubwa kwa majeraha haya ya zamani," amesema Mfalme Filipo.

Upande wake Rais Félix Tshisekedi hakutaka kuyawekea mkazo mambo ya kale, kwani anawaza kuwa yaliyo muhimu ni yale ambayo yatafanywa siku za usoni na Ubelgiji pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

MfalmePhilippe na Malkia Mathilde wa Ubelgiji wawasili DRC

"Katika majadiliano yetu hatukuyarejelea mambo ya  zamani. Tunataka kutazama wakati ujao kwa sababu wakati uliopita ni wa utukufu na huzuni. Lakini lengo hapa ni kujenga kitu kipya na cha uhakika ambacho ni cha ujenzi kwa nchi zetu mbili," amesema Félix Tshiseked.

Mfalme Philippe ajuta lakini hakuomba radhi Kongo

01:26

This browser does not support the video element.

Lakini wakongomani walio wengi walikuwa wakingojea mfalme Filipo kuomba msamaha na hata malipo kuhusu yote Ubelgiji iliyotenda dhidi yao nchini Kongo wakati wa ukoloni. 

Lazare Kanyinda, mkazi wa Kinshasa amesema "Hii ni fursa ya kuomba msamaha kwa watu wa Kongo. Wabelgiji wamefanya uharibifu mkubwa sana hapa. Kuomba msamaha haugharimu chochote ikilinganishwa na madhara ambayo Wakongomani waliyapata," huku akiongeza kuwa "ni wajibu wake kuomba msamaha."

Mfalme Filipo pamoja na mkewe Malkia Matilda na ujumbe wanaouongoza wataelekea Lubumbashi siku ya Ijumaa kabla ya kuuzuru pia mji wa Bukavu.