1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUingereza

Mfalme wa Uingereza Charles III ahudhuria ibada ya misa

11 Februari 2024

Mfalme Charles III wa Uingereza leo amehudhuria ibada ya misa, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana hadharani tangu tangazo la Kasri la Buckingham wiki moja iliyopita kwamba ana saratani

Mfalme Charles III wa Uingereza akiondoka katika hospitali ya London baada ya kugunduliwa kuwa na saratani mnamo Januari 29, 2024
Mfalme Charles III wa UingerezaPicha: Alberto Pezzali/AP/dpa

Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 75 alipigwa picha akiingia katika Kanisa la St Mary Magdalene kwenye makaazi ya kifalme ya Sandringham, Mashariki mwa Uingereza, ambako anaishi kwa sasa.

Soma pia: Mfalme Charles III wa Uingereza agunduliwa na saratani

Kuonekana kwa mfalme huyo kunakuja baada ya yeye kutoa ujumbe hapo jana Jumamosi jioni akielezea "shukrani zake za dhati kwa salamu nyingi za kheri njema'' ambazo amepokea tangu tangazo la ugonjwa wake kutolewa siku ya Jumatatu.

Mfalme Charles atoa kauli ya kwanza hadharani tangu kutangazwa kuugua saratani

Charles aliongeza kuwa mawazo mazuri kama hayo ndiyo faraja kuu.  Hii ilikuwa kauli yake ya kwanza tangu Kasri la Buckingham kusema kuwa ameanza matibabu ya "aina ya saratani," bila kutaja ni aina gani.

Soma pia. Sunak amtakia afua Mfalme Charles III anayeugua saratani

Charles amechukua mapumziko kwa muda usiojulikana ya kutekeleza majukumu ya umma ya kifalme lakini anaendelea kufanya kazi za kiutawala faraghani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW