SiasaUfaransa
MFS: Ufaransa na Italia huwanyanyasa wahamia
4 Agosti 2023Matangazo
Kwenye Pwani ya Mediterania wanakabiliana na mateso makubwa kutoka kwa polisi wa Ufaransa huku Italia ikiwapa msaada hafifu na kukosa huduma muhimu.
MSF imesema Ufaransa imekuwa ikiwarejesha moja kwa moja nchini Italia wahamiaji wote wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria, na mara nyingi hutumia mabavu, unyanyasaji na kuwazuia watu kiholela. Serikali ya Paris na Rome zote hazijatoa maoni kuhusu ripoti hiyo.
Kwa muda mrefu, suala la uhamiaji limekuwa kiini cha msuguano katika mahusiano kati ya Ufaransa na Italia huku kukiwa na mvutano ndani ya Umoja wa Ulaya kuhusu sera inayofaa ili kushughulikia vitendo vinavyoongezeka vya wahamiaji wanaotaka kuingia Ulaya hasa wakitokea Afrika Kaskazini.