JamiiMamlaka ya Palestina
Mfungwa maarufu wa Kipalestina afariki baada ya kugoma kula
2 Mei 2023![Trauer um Khader Adnan, einem palästinensischen Gefangenen, der im israelischen Gefängnis starb](https://static.dw.com/image/65487783_800.webp)
Matangazo
Tukio hilo limekuja katika wakati ambapo tayari mvutano umeongezeka kati ya Israel na Wapalestina.
Kifo cha Adnan kimeongeza uwezekano wa kuzuka upya machafuko kati ya Israel na makundi ya wanamgambo ya Kipalestina wakati vurugu zikiongezeka katika Ukingo wa Magharibi.
Muda mfupi baada ya kifo cha mfungwa huyo kutangazwa, wanamgambo Wakipalestina katika ukanda wa Gaza walifyetuwa maroketi kuelekea Kusini mwa Israel.
Aidha wapalestina wameitisha mgomo mkubwa katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza na maandamano yanatarajiwa baadae leo.
Khader Adnan aliyekuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo la Jihad ndani ya Palestina ni mfungwa wa kwanza kufa tangu wafungwa wakipalestina kuanzisha mgomo wa kula katika kipindi cha kiasi muongo mmoja.