Mgogoro kuhusu umilikaji wa visiwa baina ya China na Japan
18 Septemba 2012Matangazo
Maandamano hayo, mingine ya hamasa kubwa na yakipita mbele ya ubalozi wa Japan mjini Beijing, yamezusha wasiwasi wa kimataifa na hofu baina ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani. Kuna ripoti kwamba makampuni ya kijapani hivi sasa yanafungwa au kupunguza shughuli zao huko China.
Othman Miraji alizungumza na mwandishi wetu wa Beijing, Fadhili Mpunji, na akamuuliza uhasama huu unaangaliwa kwa kiasi gani huko China.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mahojiano: Othman Miraji/ Fadhili Mpunji
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman