Mgogoro wa kisiasa wazidi kutanuka Iraq
23 Agosti 2022Matangazo
Hatua hiyo imeelezwa kuwa mgogoro mkubwa tangu uvamizi wa Marekani.
Katika siku za hivi karibuni kiongozi huyo amesababisha uwepo wa hali ya wasiwasi kwa kuamuru maelfu ya wafuasi kuvamia na kudhibiti bunge, na hivyo kuzuia uundwaji wa serikali ikiwa takribani miezi 10 tangu kufanyika kwa uchaguzi.
Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi, ambaye amekatisha ziara yake nchini Misri ili aweze kushughulikia mgogoro huo, amezitaka pande zote kuwa tulivu na kurejea wito wake wa mazungumzo ya kitaifa.