Mgogoro wa Msikiti Mwekundu nchini Pakistan.
9 Julai 2007Matangazo
Waziri Mkuu bwana Shaukat Azizi amesema kuwa sheikh huyo ataruhusiwa kuonana na mama yake ikiwa atasalimu amri. Hatua hiyo inafuatia uamuzi wam rais
Rais Pervez Musharraf kumteua aliekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kusuluhisha katika mgogoro huo ambapo watu 24 tayari wameshauawa tokea uanze.
Waziri mkuu wa Pakistan bwana Shukat Azizi amefahamisha kwamba serikali itamruhusu sheikh Abdul Rashidi Ghazi kuwekwa chini ulinzi nyumbani alipo mama yake mgonjwa ikiwa atasalimu amri na kuwaachia wanawake na watoto anaowashikilia ndani ya msikiti.
Leo ni siku ya saba tokea waislamu hao wenye itikadi kali wamekuwa wanawashikilia wanawake na watoto hao ndani ya msikiti huo katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad.
AM.