Mgogoro wa Ukraine waendelea
6 Aprili 2007Matangazo
Bwana Viktor Yanukovych amesema kuwa hatua iliyochukuliwa na rais wa Ukraine bwana Yushenko ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mapema si halali.
Akizungumza na wandishi habari bwana Yanukovych alisema kuwa rais Yushenko amekiuka katiba kwa kuitisha uchaguzi mapema.
Waziri mkuu Yanukovych amesema ili kuepusha mgogoro kuendelea kushtadi ameiomba Austria iiingilie kati ili kusuluhisha.
Na ABDU MTULLYA