1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea urais Tunisia ahukumiwa miaka 12 jela

1 Oktoba 2024

Mgombea uraisi kwa tiketi ya upinzani nchini Tunisia amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela baada ya kutiwa hatiani kwenye mashitaka manne, likiwemo la kughushi kura zilizomuidhinisha kuwa mgombea wa urais.

Bango lenye picha ya mgombea urais aliyehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela, Ayachi Zammel.
Bango lenye picha ya mgombea urais aliyehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela, Ayachi Zammel.Picha: Fethi Belaid/AFP/Getty Images

Wakili wa Ayachi Zammel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba bado mwanasiasa huyo anabakia kuwa mgombea katika uchaguzi huo wa rais unaofanyika siku ya Jumapili (Oktoba 6).

Soma zaidi: Makumi ya wanachama wa Ennahda wakamatwa kuelekea uchaguzi Tunisia

Zammel ambaye ni mbunge wa zamani na mfanyabiashara anaongoza chama kidogo cha kiliberali na amekuwa ni mmoja kati ya wagombea wawili walioidhinishwa na Tume ya Uchaguzi ya Tunisia kupambana na Rais Kais Saed katika uchaguzi huo wa rais.

Tume ya uchaguzi imewazuia kiasi cha wagombea wengine 14 kuwania kwenye uchaguzi huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW