1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Mgombea wa chama tawala Senegal akubali kushindwa

25 Machi 2024

Mgombea wa chama tawala nchini Senegal Amadou Ba ametambua ushindi wa mgombea wa chama cha upinzani Bassirou Diomaye Faye, katika duru ya kwanza yá uchaguzi wa rais na kutoa pongezi zake.

Senegal | uchaguzi 2024
Mgombea wa urais Senegal Bassirou Diomaye FayPicha: Abdou Karim Ndoye/REUTERS

Ba amesema kwa kuzingatia mwelekeo wa matokeo ya uchaguzi wa rais, na wakati wakisubiri tangazo rasmi, anampongeza Faye kwa ushindi wake katika duru ya kwanza. 

Wafuasi wa Faye mapema walianza kusherehekea katika barabara za mji mkuu wa Senegal, Dakar mara baada ya vyombo vya habari vya ndani vilipoanza kutangaza hesabu za kura kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.

Faye ameahidi mabadiliko makubwa nchini Senegal na kugawa upya raslimali za taifa hilo kwa usawa, iwapo atashinda uchaguzi huo. 

Senegal: Faye akaribia ushindi katika uchaguzi wa rais

Faye mwenye umri wa miaka 44, aliahidi pia kuanzisha sera za Kiafrika za mrengo wa kushoto, na kujadili upya mikataba ya mafuta, wakati ambapo Senegal inatarajia kuanza uchimbaji wa mafuta yaliogunduliwa hivi karibuni, na hifadhi ya gesi baadae mwaka huu.

Ushindi wa mgombea huyo wa upinzani, ambaye atakuwa rais mdogo zaidi wa Senegal, huenda ukasababisha dhoruba ya kisiasa kutokana na sera zake za mageuzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW