CHAUMMA yapigania kurejesha hadhi ya bunge Tanzania
29 Oktoba 2025
Kwa sasa, Mwalimu ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho, akitokea chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, ambacho hakishiriki kwenye uchaguzi huo. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, Mwalimu alisimama kama mgombea mwenza wa Tundu Lissu, aliyewania urais kupitia CHADEMA, ambacho yeye aliwa Naibu Katibu Mkuu wake.
Mwalimu, ambaye kitaaluma ni mwanahabari, amekuwa kwenye siasa za upinzani kwa miaka mingi. Mwaka 2015 aliwania ubunge wa jimbo la Kikwajuni kisiwani Unguja, mwaka 2018 jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam, na mote kupitia CHADEMA na mote alishindwa.
Mwalimu alipigania kurejesha hadhi ya bunge
Baada ya kujienguwa CHADEMA na kujiunga na CHAUMMA mapema mwaka huu, Mwalimu amekuwa akijishughulisha na ujenzi wa chama chake kipya, akitembea kote Tanzania kusaka uungaji mkono.
Kwenye kampeni zake kuelekea uchaguzi wa leo, Mwalimu alipigania kurejesha hadhi ya bunge alilosema limegeuka kuwa chombo cha kumsifia tu rais, huku kwenye uchumi akizungumzia mikopo nafuu kwa vijana na akinamama.
Kutokana na kutoshiriki kwa vyama vikuu vya upinzani kama vile CHADEMA na ACT Wazalendo kwenye uchaguzi wa urais na udhaifu wa miundombinu ya vyama vidogo, wachambuzi wa siasa wanatarajia ushindi wa kishindo kwa Rais Samia Suluhu Hassan na CCM. Hii inamaanisha kuwa matokeo ya uchaguzi huu huenda yasitofautiane sana na utabiri wa ushindi wa mapema kwa chama tawala.