1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea wa ukansela Ujerumani amkemea bilionea Musk

30 Desemba 2024

Mwanasiasa wa kihafidhina anayetaka kuwa kansela ajaye wa Ujerumani, Friedrich Merz, amemkemea bilionea wa nchini Marekani Elon Musk kwa kuunga mkono chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD katika uchaguzi ujao.

Friedrich Merz wa chama cha CDU
Merz ameutaja wito wa Musk wa kuunga mkono AfD katika uchaguzi wa Februari 23 kuwa ni usumbufu na unaopindukiaPicha: IMAGO/Political-Moments

Mwanasiasa wa kihafidhina anayetaka kuwa kansela ajaye wa Ujerumani, Friedrich Merz, amemkemea bilionea wa sekta ya teknolojia nchini Marekani Elon Musk kwa kukiunga mkono chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani - AfD katika uchaguzi ujao.

Merz ambaye ni mkuu wa chama cha Christian Democratic Union - CDU amesema hawezi kukumbuka, katika historia ya mataifa ya Magharibi, kwamba kumekuweko na kisa cha kufafanishwa cha uingiliaji katika kampeni ya uchaguzi ya nchi rafiki. Merz ameutaja wito wa Musk wa kuunga mkono AfD katika uchaguzi wa Februari 23 kuwa ni usumbufu na unaopindukia. Katika maoni aliyoandika kwenye gazeti la kihafidhina la Ujerumani Die Welt, Musk alikielezea chama chama cha AfD kuwa cheche ya mwisho ya matumaini kwa Ujerumani. Makala hiyo ilisababisha kujiuzulu kwa mhariri mmoja mwandamizi wa gazeti hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW