Mgomo mkubwa wa sekta ya uchukuzi waitikisa Ujerumani
27 Machi 2023Matangazo
Safari za ndege, treni na hata mabasi zimeguswa na mgomo huo utakaodumu kwa saa 24 kuanzia leo, ambapo wafanyakazi wanadai nyongeza ya asilimia 10.5 ya mshahara.
Uchumi wa Ujerumani ambao ni mkubwa zaidi barani Ulaya unakumbwa na misukosuko kutokana na mfumuko wa bei. Mazungumzo ya siku tatu yamepangwa kufanyika kati ya serikali na vyama vya wafanyakazi.
Waziri wa mambo ya ndani Nancy Faeser, ambaye anawakilisha serikali ya shirikisho amesema watashiriki kunako majadiliano hayo wakiwa na msimamo thabiti, wa haki na wa kujenga.