1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa usafiri wa treni wa saa 50 Ujerumani wafutwa

13 Mei 2023

Chama cha wafanyakazi wa reli na usafiri nchini Ujerumani, EVG kimesema kimefuta mgomo wa siku tatu wa usafiri wa treni.

Berlin Hauptbahnhof Streik durch Verdi und EVG
Picha: Jochen Eckel/picture alliance

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimetangaza Jumamosi kuwa EVG  imeufuta mgomo huo wa nchi nzima baada ya kufikia makubaliano Shirika la usafiri wa reli nchini Ujerumani, Deutsche Bahn. 

Mgomo huo wa saa 50 ulipangwa kuanza Jumapili jioni na ulitarajiwa kuathiri pakubwa usafiri siku ya Jumatatu na Jumanne wiki ijayo. 

Hata hivyo, taarifa kuhusu makubaliano yaliyofikiwa bado hazijawekwa wazi. 

Awali, Deutsche Bahn liliiomba mahakama kutoa haraka amri ya kuuzuia mgomo huo kwa maslahi ya wateja. 

Shirika la Deutsche Bahn lilisema lingefuta safari zote za treni za umbali mrefu na huduma zote za usafiri wa majimbo wakati wa mgomo huo. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW