1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa wafanyakazi watatiza usafiri wa ndege Nigeria

4 Juni 2024

Mashirika ya kutetea haki za wafanyakazi ya Nigeria yameizima gridi ya kitaifa ya umeme nchini humo na kutatiza usafiri wa ndege jana.

Nigeria | Rais Bola Ahmed Tinubu
Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Sunday Aghaeze/AP Photo/picture alliance

Haya yamefanyika baada ya mashirika hayo kuanzisha mgomo uliosababisha kufungwa kwa shule na afisi za umma baada ya kushindwa kufikia maelewano na serikali kuhusiana na mshahara wa chini kabisa wanaostahili kulipwa wafanyakazi.

Mashirika hayo mawili makuu, Nigeria Labour Congress NLC na Trade Union Congress TUC yamesema yamewaamrisha wanachama wake kususia kazi baada ya serikali kukataa kuongeza mshahara wa chini zaidi kuwa zaidi ya dola 40 kwa mwezi.

Soma pia:Nigeria yaongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali

Serikali ya nchi hiyo imechapisha taarifa ikisema ina nia ya kuongeza mshahara huo wa chini kabisa na kwamba itafanya mazungumzo na mashirika hayo kila siku kuhakikisha suluhu linapatikana.

Afisi ya rais wa nchi hiyo pia imetoa wito wa mkondo wa mazungumzo kufuatwa na pande zote mbili kwa ajili ya kupatikana kwa mwafaka. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW