Mgomo wa walimu Kenya waendelea
16 Julai 2013Matangazo
Walimu hao waliopewa amri ya kurudi kazini na Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi au wafutwe kazini wameapa kutorudi hadi matakwa yao yatimizwe ikiwa ni pamoja na kulipwa mshahara na kuajiriwa kwa walimu wengine. Muungano wa walimu nchini Kenya kwa sasa uko katika mkutano wa kuzungumzia hatua ya mbele ya mgomo huu.
Serikali na muungano huo wa walimu umeshindwa mpaka sasa kuafikiana juu ya nyongeza ya walimu. Amina Abubakar amezungumza na mwalimu mmoja nchinI Kenya ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama, na kwanza alimuuliza iwapo ameingia kazini hii leo asubuhi. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman