1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wachafua sherehe za krismasi Ufaransa

Sekione Kitojo
26 Desemba 2019

Sikukuu ya Krismasi haikuleta  jibu kwa  wasafiri  nchini Ufaransa wakati  mgomo  wa  usafiri ukiingia  katika wiki ya nne, na kuharibu  mipango ya  maelfu ya  watu  waliokuwa  wakitaka kusherehekea  na  ndugu  zao.

Frankreich Generalstreik | Gare du Nord, Paris
Picha: picture-alliance/AP Photo/F. Mori

Watu  wengi  wamehangaika  katika  dakika  ya  mwisho  kutafuta njia  mbadala  wakati  maandamano  dhidi  ya  mageuzi  ya  pensheni yakishuhudia  maelfu  ya  treni  zikifutwa  ama  kucheleweshwa , na taksi, huduma  za  kusafiri  na  wenye  magari  na  mashirika  ya magari  ya  kukodi yakishindwa  kujaza   pengo  la  upungufu  wa matreni.

Maelfu ya watu wamekosa huduma ya usafiri wakati huu wa sherehe za krismasi katika miji mingi nchini UfaransaPicha: Reuters/G. Fuentes

ni  sehemu  ndogo  tu ya   treni  za  mwendo  kasi  na  treni zinazosafiri  kati  ya  miji  mikuu  zilitembea  katika  mkesha  wa sikukuu  ya  Krismasi  na  hata  treni  chache  zaidi  zilifanyakazi katika  sikukuu  yenyewe  jana. Vituo vikuu  vya  treni  mjini  Paris vilifungwa  majira  ya  asubuhi  ambapo huduma  za  kwenda maeneo  ya  mashambani  zilipunguzwa na  ni  njia  mbili  tu  kati  ya 16 za  treni , zile  ambazo  hazina  dereva  ndio  zilikuwa zinafanyakazi.

rais Emmanuel Macron  alitoa  wito  wa  suluhu wakati  huu  wa sikukuu , lakini  majadiliano  kati ya  serikali na  vyama  vya wafanyakazi  wiki  iliyopita   yalishindwa  kupata   msimamo  wa pamoja.

Treni zikiwa zimeegeshwa katika kituo cha Gare du Nord kutokana na mgomoPicha: Getty Images/AFP/J. Saget

Wagomaji waapa

Na  wagomaji  waliapa  kwamba  hakutakuwa  na  kusimamisha mgomo  wakati  wa  kipindi  hiki  cha  sikukuu  hadi  pale  maafisa watakapoondoa  mipango ya  kuunganisha  mifumo 42  ya  pensheni kuwa  mmoja.

Usafiri siku  ya  Alhamis  utaendelea  kuwa  wa  shida, ambapo ni treni  moja  kati  ya  mbili  zendazo  kasi  zitafanyakazi, njia  tano  za treni  mjini  paris  zitafungwa  na  huduma  za  treni  za   mikoani  na mijini  pia  zitaathirika.

Mazungumzo  yanapangwa  kuanza  tena hapo  Januari  7.

Waandamanaji mjini Paris wanaopinga mabadiliko ya mfumo wa pensheniPicha: Getty Images/AFP/A. Mesenge

Serikali  inasema  mabadiliko  ni  lazima  ili  kujenga  mfumo  wenye usawa  wa  pensheni.

Lakini  wafanyakazi  wengi  wanapinga  kujumuishwa  kwa  kile kinachoitwa  umri  wa  mwisho  wa  kustaafu  wa  miaka  64  ambapo watu wanalazimika  kufanyakazi  ili  kuweza  kupata  malipo kamili  ya pensheni, miaka  miwili  kupindukia  umri  rasmi  wa  kustaafu.