1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaBrazil

Mgonjwa anayeshukiwa kuwa na mpox agunduliwa Brazil

27 Agosti 2024

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Brazil, Anvisa, kimetangaza kumzuia mtu anayeshukiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa ya nyani katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Sao Paulo.

Mpox Impfung Impfstoff
Mgonjwa wa homa ya nyani akipata chanjo katika hospitali nje kidogo ya mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini.Picha: Xinhua/IMAGO

Kituo hicho kimesema kupitia taarifa kuwa, abiria aliyekuwepo katika eneo maalum kwenye uwanja huo wa ndege lililotengwa kwa ajili ya watu wanaosubiri kuomba hadhi ya ukimbizi tangu mapema mwezi huu, ameonyesha dalili zinazofanana na ugonjwa wa homa ya nyani.

Anvisa hata hivyo haikutoa maelezo juu ya sehemu alikotoka au nchi ya asili ya abiria huyo ambaye baadaye alipelekwa hospitali.

Soma pia: Papa Francis atoa mwito wa msaada zaidi kwa wagonjwa wa mpox

Wizara ya afya nchini Brazil imesema zaidi ya wagonjwa 700 waliothibitishwa kuugua homa ya nyani wameripotiwa kote nchini humo mwaka huu, ingawa hakuna hata mmoja aliyekutwa na aina mpya ya kirusi cha homa ya nyani.

Wiki iliyopita, serikali ya Brazil ilitangaza kwamba itaimarisha sheria za watu kuingia nchini humo ili kuzuia wimbi la wahamiaji wanayoitumia nchi hiyo kama ngazi ya kuingia Marekani na Canada.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW