1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgonjwa wa pili wa Ebola DRC amefariki dunia

26 Aprili 2022

Mgonjwa wa pili aliyekuwa anaugua ugonjwa wa Ebola amefariki dunia huko kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kongo Beni Ebola-Opfer
Picha: Jerome Delay/AP/picture alliance

Taarifa hiyo imetolewa na Shirika la Afya Duniani WHO, ikiwa ni siku chache baada ya mripuko mpya wa ugonjwa huo kutokea nchini Kongo.

WHO imesema uchunguzi wa vinasaba ulionyesha maambukizo mapya yalithibitishwa wiki iliyopita kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa.

Hata hivyo, maambukizo hayo hayahusiani na mripuko wa mwisho, ambao ulitangazwa mwezi Desemba. Mgonjwa wa pili alikuwa ni mwanamke na ndugu wa mgonjwa wa kwanza.

Mgonjwa huyo alianza kuonyesha dalili za Ebola mnamo Aprili 5 lakini hakupata matibabu kwa zaidi ya wiki moja. Baadaye alilazwa katika kituo cha wagonjwa wa Ebola mjini Mbandaka na kufariki siku iliyofuata.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW