1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron: Bado tunaumia miaka 10 baada ya shambulizi la Paris

13 Novemba 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema bado kuna "machungu" wakati taifa hilo linapoadhimisha kumbukumbu ya miaka 10 tangu yalipotokea mashambulizi mabaya.

Frankreich Paris 2025 | Hochrangige Gedenkzeremonie für die Opfer der Terroranschläge vom 13. November 2015
Miaka 10 baada ya shambulizi la Paris, Macron asema bado kuna machunguPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Mashambulizi hayo yaliyofanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu lililolenga migahawa na ukumbi wa tamasha la Bataclan mwaka 2015 yaliyosababisha mauaji ya watu 130 mjini Paris.

Mashambulizi hayo yalikuwa mabaya kuwahi kutokea nchini humo tangu kumalizika Vita vya Pili vya Dunia. Hali hiyo ilizua hofu kubwa miongoni mwa raia nchini humo na kuifanya serikali kuweka mikakati ya dharura ya kiusalama ambayo mengine yalipitishwa na kuwa sheria.

Shambulizi hilo lililotokea Novemba 13, 2015, lilianza kwa mshambuliaji kujitoa muhanga na kujiripua nje ya uwanja wa mpira wa Stade de France na kusababisha mauaji ya mtu mmoja dereva wa basi Manuel Dias, na baadae wanamgambo hao kushambulia kwa risasi maeneo mengine matano mjini Paris.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW