1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 100 tangu kuundwa jumuiya ya Wayahudi wa Marekani.

5 Mei 2006

Kulitolewa hongera nyingi jana huko Washington. Katika sherehe za jana za kuadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa jumuiya ya Wayahudi wa Marekani, AJC, walizungumza Rais George Bush wa Marekani, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan.

Kansela Bibi Angela Merkel akihutubia mkutano wa Jumuiya ya Wayahudi wa Marekani. Nyuma yuko Kofi Annan, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Kansela Bibi Angela Merkel akihutubia mkutano wa Jumuiya ya Wayahudi wa Marekani. Nyuma yuko Kofi Annan, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.Picha: AP

Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 1906 na Wayahudi wa Kijerumani ambao walihamia Marekani. Hivi sasa jumuiya hiyo ina wanachama laki moja na nusu. Ripota wetu wa Marekani, Daniel Scheschkewitz, ametutumia ripoti ifuatayo, ambayo inasomwa humu studioni na Rahab Fred….

Kansela Angela Merkel alipokewa kwa vifijo. Yeye alikuwa ni kansela wa kwanza wa Kijerumani kuzungumza mbele ya mkutano wa jumuiya hiyo. Kuanza kutoa hotuba alikuwa Rais George Bush ambaye alikuwa na maneno ya kutamka kuhusu kansela huyo wa Kijerumani:

I+ Yeye( anamkusudia Bibi Merkel) anafahamu nguvu za uhuru, anasema wazi na huniambia anachofikiri. Ana uwezo mzuri wa kuamua na ana nguvu za uongozi.+

Bibi Merkel aliwashukuru wenyeji wake kwa kumualika, jambo, ambalo sio la kawaida. Na hali hiyo imetokana na kuraruliwa utamaduni wa Kijerumani kutokana na mauaji ya maangamizi waliofanyiwa Wayahudi. Alisisitiza kwamba dhamana iliokuwa nayo Ujerumani kuelekea dola ya Israel imekuwa kubwa zaidi:

+Kupigania moja kwa moja haki ya kuweko Israel na pia haki ya raia wake kuishi ndani ya mipaka ilio ya usalama na amani pamoja na majirani zao ni jambo lisilotetereka katika siasa ya kigeni ya serekali zote za Ujerumani.+

Bibi Merkel aliongeza kusema kwamba kwa serekali ya Ujerumani ni jambo lisilostahamilika na kukubalika pale Rais wa Iran, Mahmud Ahmadinedschad, anapoiwekea alama ya kuuliza haki ya kuqweko Israel.

Akiwaelekea Wapalastina, Bibi Merkel alisema:

+Takwa la haki la wananchi wa Palastina kuishi katika dola yao wenyewe linaweza tu kutekelezeka kwa kuwa na amani na Israel. Kwa hivyo ninasikitika kwamba serekali ya Wapalastina inayoongozwa na Chama cha Hamas haijatambua kuifuata njia hiyo pamoja na Israe na jamii ya kimataifa.+

Alisema bila ya kuitambua haki ya kuweko dola ya Israel na bila ya kuachana na matumizi ya nguvu hakuwezi kuweko ushirikiano na Hamas.

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, aliwakumbusha wasikilizaji wake wa Kiyahudi kwamba hapa Ujerumani bado mahikalu ya Kiyahudi yanajengwa, kuna shule za Wayahudi na mwezi wa Septemba mwaka huu kiongozi wa kwanza wa waumini wa Kiyahudi, Rabin, katika mji wa Dresden atatawazwa. Alishukuru juu ya imani ambayo Jumuiya ya Wayahudi wa Marekani imeonesha kuelekea Ujerumani baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia; mfano ni kuweko programu za kubadilishana baina ya pande mbili na kuanzishwa ofisi ya jumuiya hiyo mjini Berlin. Bibi Merkel alisema jumuiya hiyo inajenga daraja baina ya pande mbili za Bahari ya Atlantik. Na kuendelea kushadidia kwamba anatumai jumuiya hiyo itaweza kuitimiza kazi hiyo kwa uzuri katika siku za mbele.

+

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW