1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 20 tangu mauaji ya Tiananmen Square

4 Juni 2009

Juni 4,1989 vuguvugu la demokrasia lilizimwa China.

Wanajeshi wa China.Picha: picture-alliance/ dpa

Miaka 20 iliopita, usiku wa kuamkia leo Juni 4, majeshji ya Jamhuri ya Watu wa China ya likandamiza wimbi la demokrasia kwa mtutu wa bunduki na kumwaya damu nyingi katika Uwanja wa Tiananmen Square.

Jeshi la China likitumia bunduki na vifaru liliwakabili wanafunzi na wasomi waliopaza sauti zao kulilia demokrasia na haki zaidi za kiraia na wakipinga rushua na kupendeleana chamani.Kandoni mwa uwanja huo wa Tianamen Square,mjini Beijing,shina la waandmanaji,mamia waliuwawa.Idadi halisi ya waliouwawa katika uwanja huo haijulikani hadi leo.Leo miaka 20 baada ya tukeo lile,mauaji ya umma wa watu yaliotokea katika uwanja wa Tiananmen Square hayakuchunguzwa.

Katika barabara ya Changanjie-inayoongoza katika Uwanja Tianamen, vifaru vikipita,wanajeshi wakifyatulia risasi waandamanaji .Katika uwanja wenyewe leo wamesheheni watalii kutoka nchi za nje na machina wakivutiwa na Ukumbusho wa muasisi wa jamhuri ya Watu wa China ,Mao-Tse Dung.

Siku ya leo huko Beijing ni siku ya kawaida tu.Hakuna ukumbusho wa siku hii wala hakuna kuweka koja la maua.Wala hakuna ubao wenye maandishi ya ukumbusho wa watu waliopoteza hapo maisha yao pale vuguvugu la dem,okrasia lilipozimwa.

Mpita njia mmoja anajiuliza:

"Juni 4 ? kulitokea nini ? Sijui.

Mwengine mpita njia alisema tu:

"Sijui hasa kilipita nini.Ninachojua ni kuwa wanafunzi fulani walishiriki katika kampeni."

Sawa na wapitanjia hao ,vijana wengi wa leo nchini China hawaelewi kilitokea nini siku ile.Hawsaarufiwi katika vitabu vya Shule wala kupitia vyombo vyao vya habari kile kilichotokea Juni 4,1989.Lakini kuwa serikali ya China, miaka 20 baadae bado huingiwa na wasi wasi ,mtu anatambua kupitia ulinzi mkali inaoweka.

Wanajeshi wengi wamewekwa katika uwanja wa Tiananmen kuliko ilivyo desturi na hata polisi wapo hapo.Askari wa usalama wasio na mavazi wanakodoa macho kinachopita.hasa kizazi kilichopita kinachokumbuka kilichotokea na kujionea kwa macho yao ,hakikusahau kwa muujibu asemavyo mkaazi wa Beijing Huamin, mwenye umri wa miaka 50.

"Sote tuliwafikiria wanafunzi na tukawaungamkono moyo mmoja kwa kuwa tuliona waliotenda ni jambo jema.Hawakutumia nguvu,lakini walikuwa mashujaa,kwani walithubutu kuiam bia serikali kile ambacho si sawa.Lakini pale serikali ilipotumia nguvu na kuhujumu,sote tulistushwa."

Ili siku ya leo ya ukumbusho pasifanyike maandamano ,vikosi vya usalama vya China vimejiandaa.Wakosoaji wa serikali ya China,waliotaka kuikumbuka siku hii na kilichopita, ama walikokotwa kuondolewa mjini Beijing au wamewekwsa nyumbani mwao kizuizini au wanachunguzwa masaa 24.Vyombo vya TV za nchi za nje, vinavyoripoti juu ya mauaji yaliopita,vinachujwa taarifa zao.Ukaguzi sawa na huo unafanywa katika mtandao ili watu wasijionee picha za visa vya wakati ule.

Kuchunguza kilipita nini siku ile, serikali ya China ni mwiko.Serikali inahalalisha kitendo chake hadi leo kuwa kililazimika kuzima uasi ule na inajitahidi ukumbusho wa juni 4 kuufuta kabisa vichwani mwa watu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW