Miaka 25 baada ya Srebrenica, Mahakama kimataifa zahitajika
11 Julai 2020Mahakama iliyomaliza muda wake ya uhalifu ambayo iliwahukumu viongozi wa Waserb wa Bosnia kama Ratko Mladic na Radovan Karadzic kuhusiana na mauaji ya Waislamu 8,000 wanaume na vijana ilisifiwa katika wakati fulani kama enzi mpya ya uwajibikaji wa baada ya vita baridi. pamoja na hayo mahakama kadhaa zilizoundwa baada ya hapo zinakabiliwa na matatizo kadhaa kama viwango vya chini vya hukumu , mashambulio ya rais wa Marekani Donald Trump pamoja na serikali zinazopinga, na shutuma za ubaguzi.
Pia zinahitaji kuanza kutoa haki kwa wahanga wa uhalifu wa enzi hii mpya kama vita nchini Syria, kukandamizaji wa watu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar na ukandamizaji dhidi ya Waiughur wa China, wataalamu wanasema.
Kumbukumbu ya Srebrenica ni kumbusho kuwa haja ya mahakama kama hizo kupambana na mauaji ya halaiki "ni kubwa kupita wakati wowote," amesema Nancy Combs, profesa wa sheria katika chuo kikuu cha sheria cha William and mary Law jimboni Virginia.
The Hague nchini Uholanzi , unaofahamika kama mji wa "amani na haki" ni mwenyeji wa mahakama hizi , kubwa kabisa ikiwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, iliyoundwa mwaka 2002 kuhukumu matukio mabaya kabisa duniani ya uhalifu.
Pia ni mji ambao una mahakama kwa ajili ya Kosovo ambayo hivi karibuni ilitoa mashitaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya rais Hashim Thaci, na mahakama kuhusu mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon rafiq hariri mwaka 2005.
Matatizo dhidi ya ICC
Lakini mahakama ya ICC hivi sasa inakabiliwa na mashambulio dhidi ya utawala wa Trump kwa kufanya uchunguzi wa madai ya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan, wakati utaratibu wa haki umegeuka taratibu kuwa kuwa wa ghali kwa Kosovo na Lebanon.
"Bila shaka mahakama hizi zinapitia katika nyakati ngumu kabisa kwa sasa," amesema Combs.
"Katika wakati huu katika historia, hali ya baadaye ya mahakama za uhalifu haijulikani."
Mahakama ya ICC pia "inapitia katika kipindi cha mzozo wa imani kwasababu mafanikio yake yamekuwa madogo mno katika kipindi cha muongo mmoja uliopita," Combs aliliambia shirika la habari la AFP.
Mahakama hiyo ilibidi kutupilia mbali kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, wakati huo huo kumwachia huru rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo na mwanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Jean-Pierre bemba na kuwa kama pigo kubwa kwa mahakama hiyo.
Licha ya mabadiliko ya hivi karibuni nchini Sudan, kiongozi ambaye alikuwa akitafutwa sana na mahakama hiyo rais wa zamani wa Sudan Omar al-bashitr bado hajapatikana na kufikishwa katika mahakama hiyo. Madai kwamba ICC ilikuwa tu inawahukumu watuhumiwa kutoka bara la Afrika pia yamesababisha shutuma za ubaguzi.