1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiRwanda

Miaka 27 jela kwa kuhusika na mauaji ya kimbari Rwanda

31 Oktoba 2024

Mahakama moja ya mjini Paris imemuhukumu kifungo cha miaka 27 jela daktari wa zamani nchini Rwanda Eugène Rwamucyo kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

Daktari wa zamani wa Rwanda ahukumiwa miaka 27 jela kwa jukumu lake katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994
Daktari wa zamani wa Rwanda ahukumiwa miaka 27 jela kwa jukumu lake katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Hukumu hiyo ilitolewa jana kwa Rwamucyo, mwenye umri wa miaka 65, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya kimbari na kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu .

Upande wa mashtaka umesema kuwa Rwamucyo pia alishtakiwa kwa kueneza propaganda dhidi ya Watutsi na kusimamia shughuli za kuwazika wahanga katika makaburi ya halaiki.

Rwamucyo amesema jukumu lake katika mazishi hayo ya watu wengi lilitokana na motisha ya kudumisha usafi na kukanusha kwamba manusura walizikwa wakiwa hai.

Aliondolewa mashtaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Katika kesi hiyo yote iliyodumu kwa mwezi mmoja, Rwamucyo amekanusha kufanya makosa yoyote.