1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 5 ya kufunguliwa mipaka Ujerumani

27 Agosti 2020

Miaka mitano iliyopita Kansela Merkel aliacha msemo maarufu Ujerumani''Wir Schaffen Das'' maana yake tunaweza.Ni msemo uliotokana na hatua yake ya kuruhusu mipaka ya Ujerumani iwekwe wazi kuruhusu wakimbizi kuingia

Deutschland Österreich Grenze Bayern Flüchtlinge
Picha: Reuters/M. Rehle

Ni miaka mitano sasa tangu Kansela Angela Merkel aruhusu wakimbizi kuingia Ujerumani. Mahmudul Haque Munshi ni mmoja wa wakimbizi waliokimbilia nchini Ujerumani. Yeye anatokea Bangladesh, ametiwa mkono wa bandia mweusi wenye vidole uliowekewa kifaa maalum cha hisia. Anaweza kukamata glasi ya juisi ya machungwa. Munshi anacheka na kuutazama mkono wake huo wa kulia huku akisema mkono huo wa bandia amewekewa wiki moja iliyopita na sasa anapaswa kuuzowea.

Mkono huo mpya wa bandia ni sehemu ya maisha yake mapya ambayo Mahmuhul Haque Munshi anayejiitambulisha kwa jina Munshi amekuwa akiishi nayo kwa kipindi cha miaka mitano nchini Ujerumani. Na maisha yake hayo ni tofauti kabisa na ya zamani aliyoishi kama mwanaharakati na mwanablogu. Kabla ya kukimbia kwake  kuja nchini Ujerumani mnamo mwezi Novemba mwaka 2015, kijana huyo wa miaka 34 kutoka Bangladesh alikuwa akiendesha vuguvugu linaloitwa Shahbag likiwa na wafuasi milioni tano nchini humo. Na Blogu yake katika mtandao inafuatiliwa na watu 500,000 na akiitumia kuitisha maandamano.

Maandamano dhidi ya wahalifu wa vita

Vuguvugu lake lilitowa mwito wa kubebeshwa dhamana wahalifu wa vita vya mwaka 1971 likisema wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria. Wakati huo Bangladesh ilikuwa kwenye mapambano ya kudai uhuru wake ikiijulikana kama Pakistan ya Mashariki ikiwa ni sehemu ya Pakistan.Katika vita hivyo walikufa kiasi watu milioni tatu. Leo hii mwanaharakati huyo wa zamanai wa siasa na aliyepata hifadhi ya ukimbizi na familia yake anaishi katika mji wa Düren karibu na jiji la Köln. Pamoja na mkewe Rupali Khatun wanamiliki kampuni ya mtandao ya kuagiza vitu. Na mwishoni mwa mwaka huu anaweza kutuma maombi ya kibali kitakachomuwezesha kuwa na ukaazi kamili wa kudumu nchini Ujerumani. Kwa maneno mengine atakuwa anayo haki ya kubakia kabisa nchini Ujerumani. Munshi anasema "Nchini Ujerumani kila mmoja anapaswa kuwa na mipango mizuri.''

Yeye mwenyewe anajishughulisha na mipango chungunzima kwa wakati mmoja.Anajipatia fedha ,anasomea kazi anawasaidia wakimbizi wengine na kuwa raia wa Ujerumani.

Maandamano ya vuguvugu la Shahbag mjini Dhaka. Unayemtazama mgongo ni MunshiPicha: Shahbag Movement

Mkewe Rupali aliyeanzisha kampuni ya kutuma bidhaa kupitia mtandao inayoitwa Artyship anatumai kwamba Munshi baada ya kukamilisha mafunzo kwa kufanikiwa katika kampuni moja ya utengenezaji tovuti  anataka kuwa mtaalamu wa masuala ya Kompyuta kwa ajili ya kusimamia maendekeo au mfumo wa ujumuishaji  wageni. Wazo la kuanzisha kampuni ya kutuma bidhaa aliipata baada ya kutembelea duka moja la mauzo ya jumla ya viatu vya Nike karibu na mji wa Kerpen. Munshi anasema,

''Nchini Bangladesha hakuna maduka maalum ya kuuza viatu vya Nike tu lakini kuna watu wengi wanaotaka sana viatu hivyo'' na kwahivyo mkewe na yeye mwenyewe binafsi akaanza kuwaarifu watu kupitia mtandao wake wa Facebook kwamba anayetaka viatu hivyo  nchini Bangladesh kutoka Kerpen Ujerumani awasiliane.

Bila shaka pia kuna maduka chungunzima ya raba aina ya Sneaker katika mji wa kibiashara wa Dhaka wenye wakaazi milioni 9. Lakini kununua au kupata viatu hasa kama hivyo kupitia mtandao  hilo ni jambo liloonekana kuwaavutia wengi nchini Bangladesh.Anasema

''Sina tatizo na suala hilo,kwakuwa linanipatia fedha za Wabangladesh matajiri'' Ndoto yake ni kwamba hivi karibuni afanikiwe kuhamia katika nyumba kubwa huku akisema mwanawe wa kiume ana vitu vitu na anahitaji kuwa na chumba chake''

Alikuwa kwenye Orodha ya watu wa kuuwawa

Mwanaharakati huyo wa zamani wa siasa ana mtoto wa miezi 18 Nirban Munshi na anajivunia sana. Mtoto huyo ni nembo ya maisha mapya kwa Munshi. Maisha ya mbali kabisa na maandamano ya watu wachache na ya umma mkubwa. Lakini kikubwa zaidi ni kuwa mbali kabisa na mashambulizi ya mabomu na mashambulizi ya mauaji yanayofanywa dhidi ya wafuasi wa vuguvugu la Shahbag. Vuguvugu ambalo viongozi wake wakiwekwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kuuwawa na makundi ya itikadi kali ya Bangladesh ambayo yanawaona kama watu waliolaaniwa.

Picha: DW/A. Prange De Oliveira

Munshi anasema alipokuwa nyumbani nchini Bangladesha hakuweza kuanzisha familia ambayo wakati wowote wangeuwawa. Hofu ya kuandamwa na mashambulizi ya kumuua inamuandama hadi nchini Ujerumani  ambako ameshapata vitisho vya kuuwawa mara chungunzima kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Alipoingia Ujerumani Novemba mwaka 2015 akiwa katika kituo cha kuwaweka wakimbizi katika mji wa Detmold eintraf katika jimbo la NorthRhine Westphalia,baadhi wa watu kutoka nchini mwake walimpa vitisho. Anakumbuka kwa kusema

''kila mmoja alimfahamu.Na wangeweza kuniuuwa usiku nilipolala kwasababu mtu hakuweza kufunga mlango wa chumba alicholala.Nilikuwa na mfadhaiko na mshtuko na ilibidi nipelekwe Hospitali''

Kutoka kwenye ukimbizi hadi  msaidizi

Kwa msaada wa taasisi ya Heinrich-Böll-Stiftung na shirika la kuwasaidia wakimbizi la Atheist Refugee Relief,walimsadia kupata nyumba katika mji wa Düren yeye na mkewe wakati huo.Januari mwaka 2018 mwanawe wa kiume Nirban akazaliwa. Na hivi sasa Munshi anajishughulisha  katika shirika hilo linalosaidia wakimbizi la Atheist Refugee Relief.Mnamo mwezi Mei mwaka huu alipata nafasi ya kusimamia shirika la msaada kwa wakimbizi mjini Köln. Kazi yake anawadindikiza wakimbizi wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kuzungumza lugha ya kijerumani,katika ofisi za ajira au anawasaidia kutafuta nyumba. Sasa wamekuwa wanachama wa shirika,wafanyabiashara na wazazi wa kujivunia,Munshi na mkewe Rupali Ujerumani wameshafika. Mwanablogu huyo kwahivyo ana picha ya kusimulia.

''Bangladesh ni nyumbani nilikozaliwa na kukulia.Ujerumani kwangu mimi ni kama baba kuna usalama na msaada mkubwa''

Mwandishi: Prange, Astrid/Saumu Mwasimba

Mhariri: Grace Patricia Kabogo

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW