1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Namna AU inavyotishiwa kushindwa jukumu lake la upatanishi

Iddi Ssessanga Antonio Cascais
25 Mei 2023

Shirika la Umoja wa Afrika, OAU, mtangulizi wa Umoja wa Afrika, AU, lilianzishwa miaka 60 iliyopita. Waangalizi wanalalamika hata hivyo kwamba shirika hilo limekuwa kama mbwa anaebweka tu lakini hana meno ya kung'ata.

Äthiopien 60. Jahrestag der Afrikanische Union (AU)
Picha: Solomon Muchie/DW

Ilikuwa ni zama za mwamko. Mataifa mengi ya Kiafrika ndiyo kwanza yalikuwa yamepata uhuru wake, na kuasisiwa kwa umoja huo tarehe 25 Mei 1963, ilikuwa ishara ya ukombozi wa watu waAfrika na matumani yao ya mustakabali wenye furaha.

Sehemu kubwa ya hisia hizi  za matumaini ilikuwa inahisiwa katika hotuba: "Lazima tuungane sasa au tuangamie," Rais wa kwanza wa Ghana Kwame Nkrumah alisema. Muhimu wakati huo: Uingiliaji wa kigeni unapaswa kumalizika, na Afrika iliyoungana inapaswa kuwa na sauti yeyne nguvu katika jukwaa la kimataifa.

Miaka 60 baadae, chombo kilichoirithi OAU - Umoja wa Afrika, AU- kimekuwa kikipokea lawama nzito za mara kwa mara, kikitajwa kama shirika linalowakilisha tu maslahi ya wenye nguvu, na kulaumiwa kukosa mamlaka na ufanisi na umedhihirisha kukosa uwezo wa kuleta ustawi, usalama na amani kwa Waafrika wote, ukosoaji ambao unaweza kusikika katika muktadha huu au unaofanna kote Afrika.

Hakuna amani, hakuna usalama Afrika

Wawakilishi wa mashirika ya kiraia mara kwa mara wanasema ni nadra kwa AU kulitendea haki jukumu lake la kuhakikisha amani na usalama katika bara hilo. Prof. Adriano Nuvunga, mwenyekiti wa kituo cha demokrasi na maendeleo cha nchini Msumbiji, CDD, anasema, Umoja wa Afrika haujashughulikia migogoro ya Sudan, Tigray au Sahel kwa dhamira ya kutosha. 

Shirika la zamani la Umoja wa Afrika ambalo sasa ni Umoja wa Afrika, limeadhimisha miaka 60 tangu kuasisiwa kwake. Lakini wachamabuzi wanahisi AU haina meno.Picha: Solomon Muchie/DW

Soma pia: Maadhimisho ya miaka 60 tangu kuundwa kwa Umoja wa Afrika Huru

AU pia inaahirisha kutatua mgogoro katika eneo la Cabo Delgado kaskazini mwa nchi yake ya Msumbiji, ambayo inatishiwa na wapiganaji wa itikadim kali: "Kwa sasa kuna mizozo ya kivvita katika takriban nchi 20 barani Afrika. Lakini Umoja wa Afrika hauonekani kujisikia kuwajibika. Unaonekana kulemewa." Kwa kuzingatia hili, mwanaharakati huyo anauliza: "Je, AU inaweza kufanyiwa mageuzi hata kidogo, au tunapaswa kufikiria kuhusu kuanza upya?"

Ujerumani yaiona Afrika kama mshirika muhimu

Lakini Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alielezea mtazamo tofauti kabisaa wakati alipofanya ziara nchini Ethiopia na Kenya mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei. Akizungumza katika mkutano wa waandishi habari mjini Addis Ababa, Scholz aliibua wazo la Umoja wa Afrika kuwa na kiti katika G20, ambalo ni kundi la mataifa 19 yenye nguvu kiuchumi pamoja na Umoja wa Ulaya, ambalo limekuwepo tangu mwaka 1999.

"Kuna mataifa kadhaa ambayo yameonyesha katika mazungumzo nami kwamba yanaunga mkono kiti kama hicho, na nina hakika kabisa kwamba pendekezo langu linaweza kutekelezwa haraka iwezekanavyo," Scholz alisema baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya AU Moussa Faki Mahamat.


Ukweli ni kwamba Umoja wa Afrika una nguvu kubwa kwenye makaratasi, hasa ukizingatia idadi ya wakaazi ambao shirika hilo linawakalisha kinadharia, ambao ni takribani watu bilioni 1.4. Hii leo, mataifa yote 55 ya bara hilo yanayotambuliwa kimataifa ni wanachama wa Umoja wa Afrika.

Matatizo ya AU ni yale ya mashirika ya kimataifa

Julai 9, 2002 Umoja wa Afrika ulizinduliw ana kuchukuwa rasmi nafasi ya shirika la Umoja wa Afrika OAU, lililoundwa mwaka 1963. Hafla hii ilifanyika mjini Durban, Afrika Kusini.Picha: AP

Lakini je, Umoja wa Afrika unetekeleza malengo yake ya kuhakikisha ustawi, usalama na amani? Jumbe za amani ambazo wanajeshi wa Afrika wanashiriki zimeonekana kukosa ufanisi, anasema Hager Ali, mtaalamu wa Afrika Kaskazini kutoka taasis ya utafiti wa Afrika ya GIGA ya mjini Hamburg katika mahojiano na DW.

Lakini anaweka wazi: "Tatizo la kutokuwa na meno kwa Umoja wa Afrika linatokana na mambo ambayo pia yapo katika mashirika mengine ya kimataifa." "Kwa mtazamo wa kisheria, mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Afrika hayawezi na haipaswi tu kukwepa mamlaka ya mataifa mengine ili kuingilia kati mizozo kwa uvamizi zaidi au kuitatua."

Hasa kutokana na historia ya ukoloni, pia haipendelewi hata kidogo kwa kikosi cha nje kama Umoja wa Afrika kuingilia kati serikali, haswa kwa sababu huko nyuma nguvu za kikoloni ziliwanyima watu uhuru wa kujitawala wenyewe barani Afrika, anasema Hager Ali.

Kilichobaki ni jukumu la mpatanishi

Mara kwa mara, AU imekuwa ikikosolewa kwa kutoonyesha kuguswa na vita na migogoro, kwa mfano huko Tigray, Mali au Sudan. Katika jimbo lenye matatizo la Ethiopia la Tigray, Umoja wa Afrika umejaribu kuchukua nafasi ya upatanishi. Hata hivyo, chama cha Tigray People's Liberation Front, TPLF, kimekataa mara kadhaa Umoja wa Afrika kuwa msuluhishi. Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Addis Ababa, lilisemekana kuwa na upendeleo mkubwa. Baada ya yote, mazungumzo yalifanyika Novemba 2022 kwa mwaliko wa Umoja wa Afrika, ambayo yalisababisha kusitishwa kwa mapigano.

Mtaalamu wa GIGA Hager Ali anasema: "Kulingana na sheria zake, Umoja wa Afrika hauwezi na haupaswi kufanya zaidi ya jukumu la upatanishi na kusaidia katika usimamizi wa migogoro. Hii inatumika pia kwa operesheni za ulinzi wa amani wakati AU inapojihusisha kijeshi."

Soma pia: Umoja wa Afrika kuanzisha mchakato wa maridhiano Libya

Operesheni za ulinzi wa amani, ambapo Umoja wa Afrika ulihusika katika nchi za Sudan na Mali, hazikuwa na madhumuni ya kusuluhisha migogoro ya kikanda juu ya wakuu wa nchi, lakini zaidi ya yote ni kulinda raia na kuunda na kulinda mazingira ya mfumo wa usimamizi wa migogoro, anaeleza mtafiti huyo.

Viongozi wa mataifa ya Afrika wakiwa katika picha ya pamoja kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa. Baadhi wanauona Umoja wa Afrika kama taasisi inayoshughulikia maslahi ya wenye nguvu tu.Picha: Eduardo Soteras/AFP/Getty Images

Usitekeleze asasi za kiraia

Kujumla ni vigumu kusema iwapo Umoja wa Afrika unatimiza jukumu lake kama maptanishi wa mizozo, anasema Hager. Majadiliano hayahusu AU yenyewe, lakini iwapo na namna inaunda jukwaa na mfumo wa majadiliano kwa watendaji wengine na pande zinazozozana. Swali la iwapo majadiliano hayo yanafanikiwa au la, hilo linategemea na watendaji wenyewe.

Kile ambacho Umoja wa Afrika unaweza kushindwa kwake, hata hivyo, ni kutoanzisha mfumo huu wa mazungumzo kwa wakati - au kuwaleta wahusika wasiofaa mezani, mtaalamu huyo wa Afrika Kaskazini anaongeza: "Sasa, kwa mfano katika suala la Sudan, Umoja wa Afrika umo katika hatari kubwa ya kupuuza watendaji wa kiraia na wasio wa serikali na kutoa tu jukwaa kwa wahusika halisi wa ghasia, yaani, Mkuu wa nchi Al-Burhan na kiongozi wa vikosi vya msaada wa haraka, Mohammed Hamdan Daglo."

Wakuu wa Afrika wakubaliana kuhusu mizozo

01:50

This browser does not support the video element.

Bado ni watendaji wasio wa serikali na raia ambao wanateseka zaidi katika mzozo huu. Hii ndiyo hatari ambayo AU inakabiliana nayo katika migogoro yote ambayo wahusika wasio wa serikali wanahusika - kama vile Mali au eneo la Tigray. Mfumo wa majadiliano wa AU kila mara umeundwa kwa ajili ya watendaji wa serikali, anaelezea Hager Ali. Haya ndiyo mataifa ambayo miaka 60 iliyopita, mwanzoni mwa enzi mpya, yalikataza uingiliaji wowote wa nje.

Mwandishi: Antonio Cascais