1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich yachapwa 4-1 na Barcelona

24 Oktoba 2024

Miamba ya Ujerumani, Bayern Munich imekula kichapo cha mabao 4-1, katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona na Uhispania.

Vincent Kompany - Kocha wa FC Bayern München
Kocha wa Bayern Munich Vincent Kompany amesema wachezaji wake hawakutumia vizuri nafasi katika mechi dhidi ya BarcelonaPicha: picture alliance/Peter Schatz

Hat Trick ya Raphinha na bao la nne la Robert Lewandowski yalitosha kuwalaza miamba hao waliomaliza mtanange huo na bao pekee lililofungwa na Harry Kane.  

Kocha wa Bayern ya Vincent Kompany amesema baada ya mechi hiyo kwamba wachezaji wake walishindwa kutumia vizuri nafasi walizozipata.

Erling Haaland naye alikisaidia kikosi cha Manchester City kutoka kifua mbele kwa mabao 5-0 dhidi ya Sporta Prague, huku Liverpool ikiichapa RB Leipzig 1-0.

Meneja wa City, Pep Guardiola alilisifu goli la Haaland alilolifunga kwa ustadi mkubwa, akisema baada ya mechi hiyo kwamba goli halikuwa halikuwa la kawaida "kufungwa na binaadamu" na kulifananisha na mshambuliaji, raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovich.

"Ni vigumu kuamini hiki kipaji alichonacho Haaland," alisema Guardiola.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW