1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIAMI:Kimbunga Rita kuelekea Marekani

21 Septemba 2005

Taarifa kutoka Marekani zinasema kwamba kimbunga Rita sasa kimefikia kiwango cha pili cha nguvu ya kimbunga huku kimbunga hicho kikielekea Kusini Mashariki mwa Marekani.

Upepo mkali na mvua kubwa imeikumba eneo la Florida wakati kimbunga Rita kikielekea kaskazini mashariki na Marekani.

Tahadhari zimetolewa kwa wanaoishi kwenye maeneo ya visiwa hivyo,pwani ya kusini ya Florida na Kaskazini Magharibi mwa Cuba.

Rais Gorge Bush akitembelea mji wa Louisiana kwa mara ya tano tangu kutokea kimbunga cha Katrina ametilia mkazo kuchukuliwa hatua za mapemaza dharura za kukabilina na kimbunga Rita.

Wakati huo huo Mayor Ray Nagin wa New Orleans amefutilia mbali mpango wa kurejea kwa wakaazi wa mji huo ulioharibiwa vibaya na kimbunga Katrina wiki tatu zilizopita kutokana na hofu ya kimbunga kipya Rita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW