1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michel Platini ahojiwa na mwendesha mashitaka Uswisi .

Sekione Kitojo
31 Agosti 2020

Michel Platini nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa anashukiwa kushiriki kufanya uhalifu katika mapipo ya dola milioni 2 kutoka FIFA.

Frankreich Freilassung von Michel Platini
Picha: Reuters/G. Fuentes

Mwanasoka nyota wa zamani  wa Ufaransa Michel Platini amewasili katika  ofisi ya mwendesha  mashitaka wa  Uswisi  leo asubuhi akitakiwa kwa mahojiano juu  ya  malipo ya dola  milioni 2 aliyopokea kutoka  FIFA mwaka 2011.

Platini  rasmi ni mshukiwa kwasababu ya malipo hayo ambayo  yamepelekea  kuondolewa kwake madarakani kama  rais wa shirikisho  la  kandanda  barani  Ulaya  UEFA, na kama  mgombea wa  kiti  cha  urais wa FIFA, ambako  wachunguzi wa serikali kuu  ya  Uswisi  walifichua madai  hayo  miaka  mitano iliyopita.

Michel Platini ameitwa na mwendesha mashitaka wa UswisiPicha: Reuters/G. Fuentes

Platini nahodha wa zamani  wa  timu  ya  taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 65 anashukiwa kuwa mshirika  wa  uhalifu wa  ubadhirifu, wa matumizi mabaya ya  fedha na kitendo cha kughushi, kwa mujibu wa  nyaraka  zilizoonekana na shirika  la habari  la  Associated Press mwezi  Juni. Platini ambaye alikuwa makamu wa  shirikisho la kandanda duniani FIFA, hakutoa maelezo kuhusu kesi  hiyo leo wakati akiingia katika  makao makuu  ya  ofisi ya  mwendesha  mashitaka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW