Michezo. Afrika kusini mabingwa wa Rugby.
21 Oktoba 2007Matangazo
Afrika kusini wametawazwa kuwa mabingwa wapya wa dunia katika mchezo wa Rugby.
Afrika kusini imeshinda dhidi ya Uingereza kwa mabao 15-6 katika fainali za kombe la mchezo wa Rugby zilizofanyika mjini Paris siku ya Jumamosi. Percy Montgomery aliifungia Afrika kusini penalti nne, na kuipa ushindi huo dhidi ya mabingwa watetezi Uingereza. Afrika kusini ilishinda mara ya mwisho kombe hilo la dunia mwaka 1995.