Michezo. Ujerumani kuwa mwenyeji fainali za wanawake.
31 Oktoba 2007Matangazo
Ujerumani imeteuliwa kuwa mwenyeji wa fainali za soka kwa wanawake mwaka 2011. Rais wa shirikisho la soka la kimataifa FIFA Sepp Blatter, alitangaza hayo kufuatia mkutano wa kamati kuu ya shirikisho hilo la kandanda mjini Zurich.
Canada ni nchi pekee nyingine ambayo pia iliomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Blatter pia alitangaza kuwa Brazil imechaguliwa kuwa mwenyeji wa fainali za dunia za soka kwa wanaume mwaka 2014. Brazil ni nchi pekee iliyoomba kuwa mwenyeji baada ya Colombia kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho mwaka huu. Mara ya mwisho Brazil kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya fainali za dunia ilikuwa mwaka 1950.