1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MICHEZO YA OLIMPIK YA ATHENS YAJONGEA.BUNDESLIGA YAANZA IJUMAA HII NA CHINA NA IRAN ZAKUMBANA KESHO KATIKA NUSU-FINALI YA KOMBE LA ASIA.

Ramadhan Ali2 Agosti 2004

MICHEZO

Katika changamoto ya kujipima nguvu kabla msimu mpya wa Bundesliga kuanza,mabingwa watetezi Werder Bremen wanakumbana jioni hii na mabingwa mara kadhaa Bayern Munich, ambayo kwa msangao wa mashabiki wengi,wametoka mikono mitupu msimu uliopita.Hii iliongoza kukatiza mkataba kwa kocha wao maarufu Ottmar Hitzfeld ambao ulikuwa udumu hadi mwakani. Mahala pake, pamechukuliwa na kocha wa hadi sasa wa Stuttgart, Felix Magath.

Margath hana sifa ya kuiongoza klabu yoyote kutwaa ubingwa.Alikwishakuwa kocha wa klabu zifuatazo-Hamburg,klabu yake ya zamani, Bremen,Eintracht Frankfurt na hata Stuttgart.Iwapo yeye ataweza kurekebisha makosa ya msimu uliopita,kwani klabu ya hadhi kama Bayern Munich, haimudu tena kutoka mikono mitupu msimu wapili mfululizo.

Mlinzi wao mashuhuri mfaransa Lizarazu amewaacha mkono,lakini mkipa wao mashuhuri Oliver Kahn,mchezaji stadi wa kiungo Michael ballack na Mholanzi Roy Makaay bado watapepea bendera ya bayern Munich msimu huu tena.

Kwa mara nyengine tena kama jioni hii katika finali ya Kombe la kabla kuanza msimu, mabingwa Werder bremen watataka kuwaonesha Bayern munich kuwa watawapa tena changamoto.Mshambulizi wao mbrazil, Ailton haichezei tena Bremedn ,yeye amehamia Schalke.Ailton msimu uliopita alitia mabao 37 kwa Bremen na bila ya shaka msimu huu watamkosa.Iwapo atafaulu kutia mabao mengi kama hayo kwa klabu yake mpya ya schalke, yafaa kusubiri na kuona.

Klabu nyengine 2 zinanyatia kutwaa ubingwa-nazo ni Stuttgart na Borussia Dortmund.Kocha wa Dortmund,Mathias sammer amehamia Stuttghart,klabu yake ya zamani alikokua akicheza na aliibuka nayo mabingwa, 1992.

Klabu nyengine ya kutupiwa macho msimu huu itakua Bayer leverkusen ambayo msimu uliopita ilimaliza watatu.Leverkusen imeondokewa na mastadi wake 2 m simu huu-mlinzi mashuhuri,mbrazil Lucio amejiunga na Bayern Munich wakati mturuki Basturki amejiunga na Hertha Berlin,ambayo mwishoni mwa wiki imejivunia ufunguzi rasmi wa uwanja wao wa olimpik.

Msimu huu mpya wa Bundesliga utakosa na klabu 2 maarufu zilizoteremshwa daraja ya pili:FC Cologne na Eintracht Frankfurt.Klabu 3 mpya zilizopanda daraja ya kwanza ni Mainz 05,Nuremberg na Armenia Bielefeld.

Bundesliga inaanza basi ijumaa hii kwa changamoto kati ya mabingwa Werder Bremen na Schalke 04.

KOMBE LA ASIA LA MATAIFA:

Kesho wenyeji china wanakumbana na Iran katika changamoto ya nusu-finali ya kombe la Asia la Mataifa.katika nusu-finali ya pili,japan,mabingwa wana miadi na Bahrein,timu iliowasangaza wengi katika kombe hili.China, itakayoandaa michezo ya olimpik 2008,yataka kuiigiza Ugiriki inayoandaa Olimpik mwaka huu, kutoroka na kombe la Asia.Mapambano yote mawili ni ya kusisimua na uhasama wa m uda mrefu:endapo china ikiwika nyumbani mbele ya Iran kesho na Japan ikitoa Bahrein, basi uhasama wa historia kati ya Japan na china utaibuka katika finali jumamosi ijayo kuamua wapi kombe la Asia,2004 litaelekea.Iran imebainisha nguvu zake ilipouitimua Korea ya Kusini kwa mabao 4-3 katika mpambano wa robo-finali mwishoni mwa wiki.China inajiokuta katika hali ya lazima kuwasili finali kama mwenyeji tangu ilipofaulu hivyo,1984.Kocha wao,Mholanzi Arie Haan, ameapa kwamba timu yake itakua taabu kuishinda mbele ya mashabiki wa nyumbani 65.000 uwanjani.

Michezo ya Olimpik ya majira ya kiangazi itafunguliwa rasmi August 13 ijumaa ya wiki ijayo mjini Athens na wsanariadha kutoka kila pembe ya dunia wameshajinoa kwa kinyan’ganyiro cha medali za dhahabu,fedha na shaba.Miongoni mwale ambao wanatumainiwa sana kutoroka na medali za dhahabu bila wasi wasi mkubwa:ni Muethiopia Kenenisa bekele ambae ametamba katika mita 5000 na 10.000.

Upande wa wanawake, maria Mutola wa Msumbiji licha ya msukosuko aliopata karibuni, ni yeye anaetazamiwa sio tu na msumbiji bali na Afrika nzima kuwika tena na kutetea taji lake la olimpik.

Mita 1500 ni kinyan’ganyiro kingine kati ya wakenya na waafrika kaskazini:swali ni je, el gerouj atakuwa fit sawa sawa au la ?

Mita 3000 kuruka viunzi, ni mchezo ambao Kenya,inadai ni mali yake na lazima ishinde katika olimpik.katika ubingwa wa riadha wa dunia huko Paris, Mkenya aliechukua uraia wa Qatar aliwapokonya ushindi.Katika Olimpik,mjini Athens, wakenya watajiwinda kulirejesha taji hilo nyumbani linakostahiki kukaa.

Wamarekani wamekuwa wakitamba katika mbio za masafa mafupi-mita 100-200 na hadi 400 pamoja na mbio za kupokezana:Mara hii mastadi wao wamekumbwa na dosari ya doping-madhambi ya matumizi ya madawa kutunisha misuli:bingwa wa olimpik wa mita 100 na 200 wanawake, Marion Jones anachunguzwa kama mumewe bingwa wa rekodi ya dunia Tim Montgomery.Montgomery ameshindwa kujipatia tiketi ya kukimbia Athens na Marion Jones, alieshinda mita 100 na 200 huko sydney, amekata tu tiketi ya kuruka Long jump huko Athens.

Matarajio ya Wamarekani upande wa wanaume yapo kwa bingwa wa olimpik Mjamaica Asfa Powell aliekimbia kwa mara ya kwanza msimu huu mita 100 chini ya sek.10.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW