1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MICHEZO YA OLIMPIK YA ATHENS YARUDI LEO KATIKA MEDANI YA ASILIA HUKO OLYMPIA.WANARIADHA 2 WA UGIRIKI WAJITOA MICHEZONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA MADHAMBI YA DOPING:

Ramadhan Ali18 Agosti 2004

OLIMPIK ATHENS:

Siku ya 5 ya mashindano ya olimpik mjini Athens, Ugiriki inajionea kinyan’ganyiro cha jumla ya medali 21 za dhahabu kati ya hizo 4 kutoka hodhi la kuogolea na 2 katika kurusha gololi la chuma-Shot put, mchezo unaoirejesha michezo ya Olimpik katika medani yake ya asilia huko Olympia, miaka 1,600 iliopita.

Katika mkasa mkubwa wa madhambi ya doping katika olimpik tangu kisa cha Mkanada Ben Johnson,Seoul, 1988, wanariadha 2 wa Ugiriki waliotuhumiwa kukwepa uchunguzi wa madhambi ya doping wamejitoa leo michezoni na mmoja wao- Keterina Thanou ameamua kustaafu kabisa.

Mashindano ya riadha ya Olimpik yanarudi leo katika shina lake la asilia-Olympia.Kwa mara ya kwanza tangu kupita zaidi ya miaka 1,600 mashindano ya riadha-yale ya kurusha gololi la chuma yanafanyika leo huko Olympia, mbali kabisa na mji wa Athens.Hii inawapa watazamaji mlinganisho kati ya medani ya asilia ya olimpik na ya kimambo-leo mjini Athens.

Ijumaa hii , riadha itahamia katika uwanja mkuu wa Olimpik wa Athens ambamo majogoo wa Afrika , ambao hawakusikika hadi sasa wataanza kinyan’ganyiro chao cha medali za dhahabu,fedha na shaba wakitazamiwa kutia fora kuanzia mita 800 hadi marathon.

Siku ya leo lakini , ilikua siku ya kuamua hatima ya wanariadha wawili wa Ugiriki-mmoja wao shujaa wa michezo,bingwa wa olimpik wa medali ya dhahabu wa mita 200 Kostadinos Kenteris na mwenzake wakike –bingwa wa medali ya fedha wa Olimpik Ekterini Thanou. Baada ya kufika mwishoe hii leo mbele ya Kamati ya nidhamu ya Halmashauri Kuu ya Olimpik mjini Athens kujieleza ilikuaje walikwepa uchunguzi wa doping ijumaa iliopita, Kostas Kenteris na Katerina Thanou walijitoa kutoka michezo hii ya olimpik.Keterina alifika umbali kunadi kwamba anavunja kabisa ushirikiano na kocha wake Christos Tsekos.

Hii ni kashfa kubwa kabisa ya madhambi ya doping-matumizi ya madawa kuengeza kasi na kutunisha misuli tangu kisa cha Mkanada Ben Johnson ,alieshinda mbio za mita 100 huko Seoul, 1988 na kutimuliwa kwa fedheha kubwa nje ya kijiji cha olimpik.

Bingwa mwengine wa dunia maarufu alieanguka mateka wa madhambi ya doping, ni msichana wa Marekani, Torri Edwards .Msichana huyu amekataliwa rufaa yake kupinga marufuku ya miaka 2 ya kushindana .Marufuku bhayo alipigwa kwa kugunduliwa na madhambi ya doping huko kisiwani Martinique,April, mwaka jana hayafutwa.

Medali 4 za dhahabu zinaaniwa leo kutoka mawimbi ya hodhi la kuogolea na macho yote yatakodolewa katika mashindano ya kusisimua ya mita 100 –mtindo wa freestyle yatakayowakumbanisha madume 2 uso kwa uso Ian Thorpe wa australia na Pieter van den Hoogenband wa Holland.

Michael Phelps wa Marekani ameshatia medali yake ya 3 ya dhahabu mfukoni hii leo kufuatia ushindi wake wa mbio za majini za mita 200 mtindo wa kipepeo-butterfly na katika kuisaidia Marekani kuilaza Australia katika mashindan o ya kuogolea ya mita 200X4 kupokezana mtindo wa freestyle.Phelps akitazamiwa kukusanya medali 7 hadi 8 za dhahabu kutoka Athens lakini amepata pigo kutokana na ushindi wa waafrika Kusini.

Nje ya medani ya olimpik mjini Athens, jioni ya leo itajionea changamoto kadhaa za dimba kwa timu za taifa kuanzia Ulaya, Afrika hadi Amerika Kusini-baadhi ni za kuania tikiti za finali ya kombe la dunia linalokuja 2006 na baadhi ni mapambano ya kirafiki:

Ujerumani kwa mara ya kwanza chini ya kocha na nahodha mpya:Jürgen Klinsmann na Michael Ballack inacheza na Austria mjini Vienna.Uingereza ina miadi na Ukraine na Haiti na mabingwa wa dunia-Brazil.

Barani Afrika ,Algeria inakutana na Burkina Faso, Tunisia na Bafana Bafana mjini Tunis na Zambia na Simba wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, mjini Lusaka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW