Michuano ya African Football League yaanza Tanzania
20 Oktoba 2023Uzinduzi huo uliotarajiwa kupambwa na burudani za aina mbalimbali huku Uwanja wa Benjamin Mkapa, uliokuwa umefungwa kwa miezi kadhaa kwa ajili ya kupisha ukarabati, ukiwa tayari umeanza kufurika mashabiki wa Simba baadhi yao wakiwa wamesafiri kutoka mikoani.
Huo ni mchezo wa kukata na shoka na uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote mbili, lakini mashabiki wenyeji walikuwa na matumani ya kuishangaza Afrika kwa kuondoka na ushindi dhidi ya miamba hiyo ya Misri iliyowahi kutwaa ubigwa klabu bingwa barani Afrika mara 11.
Soma zaidi:
Rangi nyekundMichuano ya "SportPesa Super Cup" yaanza Daru na nyeupe zilihanikiza kila sehemu ya jiji la Dar es Salaam siku ya Ijumaa (Oktoba 20), ambako mazungumzo yote yalikuwa ni kuhusu mchezo huo uliotarajiwa kuanza saa 12:00 jioni kwa majira ya Afrika Mashariki.
Matumaini ya Simba
Licha kwamba mashabiki wa Simba kufahamu fika ubora na uwezo wa timu wanayokabiliana nayo, lakini hilo halikuwafanya waishiwe na tambo mdomoni.
Simba kwa muda wa juma nzima imekuwa na shamra shamra kuelekea katika mchezo huo, ikijinadi kuwa ilidhamiria kuandika rekodi ya aina yake kwa kuwa timu ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kushiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo ambayo pia ni mara ya kwanza kuanzishwa barani Afrika.
Msemaji wa timu hiyo, Ahmed Ally, ndiye anayepuliza baragumu zaidi la tambo akisema "kama ilivyokuwa mwiko wa toroli kupanda mlima ndivyo itakavyokuwa kwa timu yake kuacha pointi tatu zikiondoka kwenda Misri."
Mechi ya kwanza ya African Football League
Idadi ya mashabiki waliolipia kuhudhuria mechi hiyo ilitajwa kupindukia uwezo wa uwanja wa Mkapa, hali iliyolifanya jeshi la polisi kutoa tahadhari ya mapema.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, aliwaonya mashabiki wanaokusudia kufika uwanjani hapo wakiwa na silaha ya aina yoyote kuacha mara moja.
Hadi kufikia asubuhi ya Ijumaa, watu mashuhuri wa soka walikuwa wameshawasili kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa michuano ya ligi hiyo, ambayo ni mara ya kwanza kuanzishwa barani Afrika ikiijumuisha timu nane.
Wageni zaidi walitarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo, akiwamo Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, na pia aliyewahi kuwa kocha wa klabu ya Arsenal ya England, Arsene Wenger.